Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Muheza alipofika katika Mahakama hiyo kwa ziara ya kikazi aliyoanza jana tarehe 16 Mei, 2022.
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama wakiandika masuala mambo ambayo alikuwa akizungumza Jaji Mkuu, Mhe. Prof. Juma (hayupo katika picha) alipokuwa wilayani Muheza kwa ziara ya kikazi.
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Muheza wakimsikiliza Mhe. Prof. Juma alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea Mahakama hiyo kwa ziara ya kikazi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Juma akionyesha fomu maalum ya Mahakama kwa ajili ya kutoa maoni wakati alipokuwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu wa Mahakama Wilaya ya Muheza alipotembelea Mahakama hiyo. Kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Tanga, Mhe. Latifa Mansoor na kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Kevin Mhina.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu wa Mahakama Wilaya ya Pangani alipotembelea Mahakama hiyo. Kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Tanga, Mhe. Latifa Mansoor na kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Kevin Mhina.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Ghaibu Lingo (wa tatu kushoto) mara ya Jaji Mkuu, Mhe. Prof. Juma kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Tanga, Bw. Humphrey Paya pamoja na Watumishi wengine wa Mahakama na Watumishi/Wadau wa Ofisi hiyo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhe. Halima Bulembo (wa pili kushoto) mara ya Jaji Mkuu, Mhe. Prof. Juma kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo. Wa pili kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Tanga, Mhe. Latifa Mansoor, wa kwanza kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin Mhina na wa kwanza kushoto ni Naibu Msajili wa Kanda hiyo, Mhe. Beda Nyaki.
……………………………………..
Na Mary Gwera, Mahakama-Tanga
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewahimiza Wadau wa mnyororo wa utoaji haki nchini kusoma hukumu zinazotolewa na Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ambazo zimesheheni mambo muhimu yatakayosaidia kurahisisha utoaji wa haki kwa wananchi ikiwa ni pamoja na namna bora ya kushughulikia mashauri ya Mirathi na ya dawa za kulevya.
Akizungumza kwa nyakati tofauti siku ya kwanza ya ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama Kanda ya Tanga aliyoianza jana tarehe 16 Mei, 2022 akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Wilaya ya Pangani, Mhe. Prof. Juma alisema kuwa kwa kufanya hivyo itapunguza baadhi ya makosa yanayofanywa na wadau wakiwemo waendesha mashtaka na wananchi kwa kutojua sheria na kanuni zinazosimamia mashauri mbalimbali.
Comments
Post a Comment