RAIS SAMIA AIPONGEZA WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KWA UBUNIFU
Na John Mapepele Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu ameipongeza Wizara ya utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kazi kubwa inayofanya ya kuitangaza Tanzania duniani kupitia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Samia ametoa kauli hiyo wakati akipokea Kombe la Dunia la FIFA leo Mei 31, 2022 Ikulu jijini Dares Salaam kutoka kwa kiongozi kikosi cha ziara ya kombe hilo hapa nchini na mchezaji nguli wa Brazil Juliano Belletti. Amesema Wizara hiyo imekuwa ikifanya ubunifu mkubwa wa kuitangaza Tanzania ambapo katika siku za hivi karibuni kwa kushirikiana na wadau waliandaa tukio la kutazama mbashara fainali za UEFA kupitia DSTv kwenye Daraja jipya la Tanzanite lililopo jijini Dar es Salaam hivyo kuifanya dunia kuendelea kuilifahamu daraja hilo la kisasa na Tanzania kwa ujumla wake. "Lakini kutumia lile daraja na wakaonyesha na tukaonekana ulimwengu mzima ile ni jitihada kubwa, na wameonesha kwamba Tanzania tuna vivutio vinavyoweza ku...