Mhe. Mchengerwa- Serikali kuwashirikisha wadau kwenye mnyororo wa thamani wa utalii
Na John Mapepele Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imedhamiria kufanya kazi kwa pamoja na wadau mbalimbali wa utalii nchini kwa ajili ya kuimarisha mahusiano ya serikali na wadau (Public Private Partnership) ili kufikia kwa haraka lengo la kuwapata watalii milioni tano hatimaye kuchangia kwenye uchumi wa nchi. Akizungumza kwenye Tamasha la Kwanza la Biashara la Wadau wa Utalii leo, Februari 23, 2023 lililopewa jina la “The Z sumit” ambapo Rais wa Zanzibar, Mhe. Hussein Mwinyi amekuwa Mgeni Rasmi, Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa dhamira ya serikali kwa sasa ni kuwashirikisha wadau wote kwenye mnyororo wa thamani wa utalii ili kutoa huduma ya kiwango cha kimataifa kitakachowavutia watalii kuja kujionea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini. Aidha, amemhakikishia Mhe. Rais Mwinyi kufanya kazi kwa karibu na Waziri anayesimamia sekta ya Utalii kwa upande wa Zanzibar katik...