Ivan Edmund kutoka kampuni ya dawa za binadamu ya Philips Pharmaceuticals Tanzania Ltd. akitoa dawa kwa mwananchi aliyekutwa na tatizo la moyo mara baada ya kupata matibabu wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika jana katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Katika maadhimisho hayo wananchi walipata bila malipo huduma za Upimaji,ushauri, matibabu ya moyo na rufaa ya moja kwa moja kwa wale waliokutwa na matatizo ya moyo yaliyohitaji matibabu ya kibingwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa elimu ya jinsi gani unaweza kuepuka kupata magonjwa ya moyo kwa wananchi waliofika katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo wilya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani. Katika maadhimisho hayo wananchi walipata bila malipo huduma za Upimaji,ushauri, matibabu ya moyo na rufaa ya moja kwa moja kwa wale wali...
Posts
Showing posts from September, 2020
UN yamuunga mkono Magufuli kutokomeza ukatili wa mwanamke Ikungi
- Get link
- X
- Other Apps
Picha ya pamoja ya Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi(mwenye kilemba) na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo mara baada ya uzinduzi wa mradi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi(kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania, Zlatan Milisic baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi Na John Mapepele, Ikungi MKUU wa Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi leo amezindua miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa pamoja baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia ufadhiri wa Shirika la KOICA wa Tuufikie usawa wa jinsia kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana utakaogharimu takribani bilioni 11.5 za kitanzania ambao utatekelezwa katika Wilaya...
WORLD VISION YAWANOA WANAHABARI KUHUSU LISHE NA AFYA YA UZAZI
- Get link
- X
- Other Apps
Meneja wa Mradi wa ENRICH, Bi Mwivano Malimbwi (aliyesimama) akitoa mafunzo maalum ya malengo ya mradi huo ya utoaji wa elimu ya lishe na kuboresha afya ya uzazi kwa vijana balehe kwenye mikoa ya Singida na Shinyanga kwa waandishi wa habari ya Mkoa wa Singida (hawapo pichani) leo, aliyekaa ni mtaalam wa Jinsia na Utetezi wa Mradi Huo Tumaini Fred Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiangalia mazao ya asali na mashine ya kukamulia asali ya kikundi cha ufugaji wa nyuki mkoani Singida kinachofadhiliwa wa World Vision hivi karibuni Na. John Mapepele ,Singida Shirika la World Vision nchini limewataka waandishi wa habari kama wadau wakuu wa Shirika hilo kutoa taarifa sahihi za kazi za shirika hilo kwenye mradi wake wa ENRICH ambao unatekelezwa katika mikoa ya Singida na Shinyanga. Mradi huo unalengo la kupeleka elimu ya lishe na afya ya uzazi kwa vijana balehe vijiji...